The Orange Door

Swahili

  

Nini maana ya The Orange Door?

The Orange Door ni njia mpya ya kupata huduma kwa wanawake, watoto pamoja na vijana ambao wanakabiliana na dhuluma za familia; na familia ambazo zinazohitaji msaada na utunzaji wa watoto au vijana. Wewe hauhiitaji rufaa ili kupata msaada pamoja na usaidizi kupitia The Orange Door.

The Orange Door inaweza kufanya nini kwa ajiri yangu?

Wasiliana na The Orange Door ikiwa:
 • mtu wa karibu na wewe anakuumiza, anakutawala au kukufanya wewe uhisi hofu, kama vile mwenzi wako, mtu wa familia, mkazi wa nyumbani au mlezi
 • wewe unasumbuliwa na ulezi kutokana na migogoro ya kifamilia, maswala ya pesa, magonjwa, ulevi, huzuni au kutengwa
 • wewe unao wasiwasi na usalama na ustawi wa mtoto au mtoto mdogo
 • wewe unao wasiwasi na usalama wa rafiki au mtu wa familia.
Ikiwa wewe ni mhamiaji au mkimbizi au hauna makazi ya kudumu, sisi bado tunaweza kukusaidia. Usiogope kutafuta msaada kwa sababu ya hali yako ya uhamiaji. Huduma hii ni bure. Julisha wafanyakazi wa The Orange Door kujua kama unapendelea kujadiliana hali yako kwa njia ya simu au uso kwa uso. 

Ninahitaji mkalimani

Julisha huduma ikiwa wewe unahitaji mkalimani. Julisha huduma:  
 • namba yako ya simu
 • lugha yako
 • wakati gani mzuri wa kukuita.
Mkalimani ataweza kukupigia tena.

Je huduma ya The Orange Door inafaa kwa ajiri yangu?

The Orange Door huwakaribisha watu wa umri wowote, jinsia, na uwezo. Mapendeleo yote ya kitamaduni na kidini huheshimiwa. Ruhusu mfanyakazi ajue ikiwa wewe unapenda kufanya kazi na mfanyakazi wa kiume au wa kike. The Orange Door inafanya kazi na huduma za kitamaduni, huduma zan Watu Waliobadili Jinsia zao (LGBTI) na huduma za walemavu kukidhi mahitaji anuwai ya watu binafsi na familia. Wafanyikazi watakupa habari kuhusu chaguzi pamoja na kukuunganisha kwa huduma unazohitaji.

The Orange Door iko wapi?

Tafuta kwa kuzingatia mahali au nambari ya posta ili kupata huduma yako ya eneo. 

The Orange Door inafunguliwa mda gani?

The Orange Door inafunguliwa kutoka 9am mpaka 5pm sikum ya Jumatatu hadi Ijumaa (inafugwa siku za sikukuu).  

Ninaweza kwenda wapi wakatiThe Orange Door haijafunguliwa?

Wasiliana na huduma zifuatazo nje ya msaa haya:
 • Huduma ya Rufaa ya Wanaume kwa 1300 766 491 (8am-9pm Jumatatu-Ijumaa na 9am-5pm Jumamosi na Jumapili) (Ushauri wa simu wa wanaume wa unyanyasaji, habari na huduma ya rufaa)
 • Safe Steps ni huduma ya msaada kwa waathirika wa vurugu za familia kwenye 1800 015 188 (masaa 24, siku 7 kwa wiki). Unaweza pia kutuma barua pepe kwa Safe Steps au kutumia huduma ya msaada wa kuzungumza halisi kwenye mtandaoni 
 • Msaada wa Waathirika wa makosa ya jinai (kwa waathiriwa wote wa uhalifu na waathiriwa wa kiume wa unyanyasaji wa familia) 1800 819 817 (8am- 11pm, kila siku)
 • Laini ya Mgogoro wa Shambulio la Kigono ni kwa waathirika wa shambulio la kingogo kwenye 1800 806 292 (masaa 24, siku 7 kwa wiki) 

Ikiwa wewe au mtu mwingine yuko katika hatari ya haraka, piga simu Sifuri tatu (000) kwa msaada wa dharura.